• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

WENYEVITI, WATENDAJI VIJIJI WAPIGWA 'STOP' ASILIMIA 10 TOZO ZA MAUZIANO VIWANJA NYUMBA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI

Kurushwa hewani: July 31st, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde  amepiga marufuku tozo ya asilimia kumi inayochajiwa na wenyeviti wa vijiji na watendaji wakati yanapofanyika mauziano ya viwanja au nyumba katika halmashauri hiyo.

Agizo hilo amelitoa leo  Jumatatu July 31, 2023 wakati akifungua mafunzo ya Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha kwa Ngazi ya Kituo cha Kutolea Huduma (FFARS) kwa watendaji na baadhi ya watumishi katika Halmashauri hiyo.

Mafunzo hayo ya FFARS yatasaidia mambo mbalimbali ikiwemo kudhibiti fedha zinazotolewa na wadau au Serikali ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kutoa huduma bora kwa wananchi au jamii kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo amesema asilimia hizo wanazotoza watendaji na wenyeviti hazipo kisheria  huku akihoji wanakozipeleka.

"Niwapeni angalizo, unakuta watu wanauziana shamba au nyumba unachaji asilimia 10 unaipeleka wapi na unakatia risiti gani?" amehoji

"Wakati wananchi wanauziana shamba halafu wewe unataka asilimia 10 huoni kuwa unamuumiza mwananchi? Hiyo ni rushwa. Sasa kuanzia leo hicho kitu tuache. Tunaidhalilisha Serikali" amesisitiza.

Akizungumza katika mafunzo hayo mkurugenzi huyo amesema mafunzo hayo yatasaidia kutambua mapato na matumizi kupitia mfumo kwa urahisi.

"Baada ya mafunzo haya washiriki wataweza kuandaa malipo yote kupitia mfumo"

Pia, Mkurugenzi huyo amewaonya watumishi hao kuwa wasitumie steshenari  kutokana na unyeti wa taarifa zitakazokuwemo katika mfumo huo.

"Tusije kwenda kufanya kazi hizo katika steshenari, kila kitu kinachofanyika katika serikali ni siri, tukienda katika steshenari zile usiri unakuwa hakuna tena" amesema na kuongeza;

"Lakini pia tukitumia mfumo huu utatusaidia kutambua wadau waliochangia fedha katika miradi ya maendeleo tofauti na ilivyo sasa tunapokea fedha bila kufahamu ni mdau gani ameleta fedha hizo" amesema

Ameeleza kuwa hiyo itasaidia kujua mapato katika kila chanzo ikiwemo michango ya maendeleo ambayo ni lazima iingizwe benki

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa