Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega amewataka watendaji wa kata, maafisa elimu kata na walimu wakuu kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi.
Mhe. Mbega ametoa rai hiyo wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Vwawa Sekondari chenye lengo la kufahamiana na kukumbushana watendaji hao wajibu wao.
"Ushirikiano huu ni muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo, hasa katika sekta ya elimu" amesema
Pia Mhe. Mbega amesisitiza umuhimu wa kuyaeleza mazuri yanayofanywa na Serikali ili jamii iweze kufahamu juhudi zinazoendelea kufanyika kwa ajili ya ustawi wa wananchi.
Katika maelezo yake amesema kuwa viongozi hawa wanapaswa kuwa kiungo thabiti kati ya Serikali na wananchi kwa kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi na za wakati kuhusu miradi ya maendeleo na mafanikio ya Serikali.
" Ni jukumu la kila mmoja kuyasemea mazuri ya Serikali ili kuondoa upotoshaji na kusaidia jamii kufahamu ukweli kuhusu juhudi zinazofanyika. Hii itasaidia kujenga imani ya wananchi kwa Serikali yao, kuimarisha mshikamano, na kuhamasisha utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa mafanikio".
"Mazuri kama haya yanaposemwa kwa uwazi, yanachochea ari ya maendeleo katika jamii kwa ujumla"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa