Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega, amewakabidhi sare za shule wanafunzi 120 wa Shule ya Msingi Isangu wanaotoka katika mazingira magumu.
Mkuu wa Wilaya huyo amekabidhi sare hizo leo Ijumaa Machi 21, 2025 katika shule ya Msingi Isangu zilizotolewa na Shirika la Elisha Foundation, shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi sare hizo, Mhe. Mbega aliwashukuru viongozi wa shirika hilo kwa moyo wao wa kujitolea na kujali ustawi wa watoto wa shule.
"Huu ni mfano mzuri wa mshikamano wa kijamii ambao tunapaswa kuendeleza katika wilaya yetu," alisema.
Pia, aliwasihi wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wa Elisha Foundation kwa kushirikiana na serikali katika kuboresha mazingira ya elimu.
Alisema kuwa changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya elimu zinaweza kutatuliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya serikali, sekta binafsi, na wananchi
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa