Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa ujenzi wa shule ya msingi ya kisasa mpya DR Samia Suluhu Hassan ya mradi wa BOOST iliyogharimu Shilingi Milioni Sh538.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa pongezi hizo leo Ijumaa Novemba 24, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi baada ya kuitembelea na kufanya ukaguzi katika shule hiyo.
Amesema kuwa katika mradi huo thamani ya fedha imeonekana dhahiri kwa kuwa hata ukiiangalia shule hiyo kwa macho inaonekana ina thamani sawa na fedha ziliyoletwa.
"Hongereni sana watu wa Mbozi tunatamani fedha zikiletwa thamani ya mradi iendane na fedha iliyoletwa.
Hongereni sana ofisi kama hizi niliwahi ziona UDSM Chuo Kikuu lakini leo zinapatikana katika shule za msingi" amesema
"Maeneo mengi tunayopita inaonekana kabisa hali sio shwari lakini kwa hapa niwapongeze mmeweza.
Na hii inajidhihirisha tulikotembea katika miradi wananchi wanafurahi uzuri wa miradi, hii ni zawadi kwa Mheshimiwa Rais ya kuonyesha fedha anazozitoa zinafanyiwa kazi" amesema
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa