MBOZI. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa amewahamasiha wananchi mkoa wa Songwe kulima zao la kahawa kwa kuwa zao hilo ni la mkakati na muhimu.
Waziri Mkuu huyo ametoa rai hiyo leo Jumanne Februari 14, 2023 alipotembelea kiwanda cha GDM kilichopo Mlowo wilayani Mbozi.
Amesema kuwa kwa sasa zao hilo ni biashara hivyo lotasaidia kuinua uchumi wa mkoa huo.
Kahawa ni zao la kimkakati na ni zao muhimu, leo Songwe ni zao la biashara kahawa kwetu sisi ni uchumi" amesema Waziri Mkuu na kuongeza
"Kahawa leo kwetu Songwe ni uchumi na ndio maana tunahangaika tupate mbegu bora na kufanya utafiti ili kuzalisha kwa tija. Tunahamasisha watu walime kahawa" amesitiza
Amesema ili kuwapa motisha wakulima, Serikali inafanya wakulima wapate pembejeo kwa urahisi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu huyo ambaye ni mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali ameupongeza uongozi wa Kiwanda cha GDM kwa uwekezaji na kutoa ajira kwa wananchi.
"Kilichonivutia kwa mwewekezaji huyu ni umri, ametoa ajira kwa watu wengi" amesema amemwambia Mkurugenzi wa GDM, Richard Mwangoka mwenye miaka 22 ambaye ni mtoto wa Full Dose.
Amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inawatengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji.
"Nilipata simu kiwanda cha mzawa amepewa salami nyingi na Rais Samia huyu mkurugenzi na uongozi wa kiwanda
Mh Rais anawasalimia wanajumuia ya GDM,
Mama Samia ametoa faraja kwa wawekezaji wawekezaji sio lazima wawe wazungu" amesema Waziri Mkuu huyo ambaye yupo katika ziara mkoani Songwe.
"Mh Samia Suluhu amenituma kuleta salamu anawatakia mpate heri, Nimekuja ziara ya siku tatu.
Ziara hii ni kupitia kuona mafanikio ya Dk Samia kuona pesa kama zimefanya kazi kwenye miradi ili ipate kuwahudumi"
"Salami hizi iendelee kutunza kiwanda chako pia mtaji uendelee" Amesema
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa