Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amezindua kampeni maalumu ya utoaji chanjo ya surua mkoani humo.
Uzinduzi huo umefanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyopo mjini Vwawa ambapo Seneda ametoa wito kwa azazi na walezi Mkoani Songwe kujitokeza kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo ya sindano dhidi ya ugonjwa wa Surua katika kampeni hiyo ambayo imeanza leo Februari 15 hadi Februari 18, 2024.
Seneda amesema mkoa unakusudia kuchanja watoto 199776 katika halmashauri zote tano za mkoa wa Songwe na kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa huo baada ya kuanza kujitokeza tena baadhi ya maeneo katika mwaka uliopita.
Mganga Mkuu wa Mkoa, Boniface Kasululu amesema kampeni hii itahusisha wataamu wa afya kwasababu ni chanjo ya sindano pia italenga maeneo maalumu ya kutolea huduma ikiwemo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, makanisani, misikitini pia haitazuia shughuli zingine za uzalishaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amewapongeza wananchi waliyojitokeza katika siku ya kwanza ya utoaji wa chanjo ambapo amewataka wawe mabalozi wa kuwahamasisha wengine
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa