Watoto 124 kutoka shule za msingi na sekondari kata ya Hezya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi wamepokea msaada kutoka katika Shirika la Wakinamama na Watoto (WAKINA Foundation).
Wanafunzi hao wamepokea msaada huo Ijumaa Machi 15, 2024 katika shule ya Sekondari Hezya.
Akisoma taarifa ya Shirika hilo mratibu wa shirika hilo Isdory amesema kuwa kwa mwaka 2024 Shirika liliweza kupata fedha zaidi ya Shilingi milioni 17 ambapo fedha hiyo imeweza kununua mahitaji ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ya shule
Amezitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule ya msingi Hezya, Haraka, Izumbi, Namwamgwa, Hayunyi, na Maringo na shule ya sekondari ya Hezya.
Amezitaja changamoto zinazolikabili Shirika kuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu wa jamii inayowazunguka kuhusiana na malezi ya watoto yatima hivyo kuibuka kwa wimbi la ukatili pamoja na utoro wa wanafunzi wanaonufaika na Mradi ambao wakipokea vifaa wanaacha shule.
Changamoto nyingine ni kutumia vibaya vifaa walivyopewa na baadhi ya watu kutothamini jitihada za shirika
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na viatu, sare za shule , madaftari, bima za afya, kalamu, begi za shule na sabuni za kuogea
Kwaupande wake mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya Brighton Mwambalwaswa amelishukuru shirika hiyo kwa kutoa vitu hivyo ambavyo vitawasaidia kuwafanya watulie madarasani
Pia amesisitiza utunzaji wa vifaa hivyo iliviweze kudumu na kuwasaidie
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa