Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe. George Musyani amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanatoa ushirikiano wakati timu ya Halmashauri inapokwenda kufuatilia wadaiwa wa marejesho ya mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri
Mhe. Msyani ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani la Kata la kuwasilisha taarifa za kata lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa baraza hilo la madiwani, Mwenyekiti huyo amesema kuwa Halmashauri inaanza mkakati wa kufuatilia madeni ya marejesho ya mikopo ya asilimia kumi kwa ngazi ya kata hivyo watendaji wa kata watoe ushirikiano kutokana na wao kuwafahamu wanufaika waliokopa katika ofisi zao.
"Wakati wa ufutiliaji wa hizo fedha Mtendaji hakikisha kikundi husika kinapatikana katika ofisi yako ya kata kuepusha usumbufu" amesisitiza
"Tunahitaji zoezi lifanyike ndani ya muda mfupi hivyo ukiwa kama kiongozi wa kata nenda ukawahamasishe hao watu wa vikundi waweze kufanya marejesho mapema kwa hiari. Sio sifa nzuri kwa vikundi vyetu kuanza kupelekana mahakamani wakati maridhiano yangefanyika" ameeleza
Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwataarifu kurejeshwa kwa mikopo ya asilimia kumi ambayo inawahusi Wanawake vijana na watu wenye ulemavu ambayo itaanza kutolewa rasmi Julai 1, 2024.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa