Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda ametoa wito kwa watendaji wa kata, mitaa na vijiji kuepusha urasimu katika zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa.
Bi. Seneda ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, ametoa maagizo hayo leo Jumanne Aprili 9, 2024 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya Taifa kwa Mkoa wa Songwe iliyofanyika katika Kata Mlowo.
Amesemakuwa zoezi la ugawaji lisianze kuwa na longolongo au mizinguko mizinguko kumpata Mtendaji Tena iwe shida tusingependa iwe hivyo
"Kama mwananchi atapata changamoto yoyote katika kupata kitambulisho na kama yupo kwenye orodha ya watu wanaopata vitambulisho asisite kuripoti na kutoa taarifa:
"Sisi viongozi wa mkoa, Wilaya tupo tayari kusimamia zoezi hilo ili liende vizuri ili Mkoa wa Songwe uibuke kidedea katika zoezi hili" amesisitiza
"Leo tupo hapa kushuhudia zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya NIDA katika Mkoa wetu wa Songwe. Ifahamike kwamba Taasisi ya NIDA inajukumu mahususi la kusajili na kutambua raia na wageni wote wanaokidhi vigezo vya kupatiwa vitambulisho vya Taifa. Nimefurahi kuona Taasisi ya NIDA imefanya maboresho makubwa kwenye usajili na utambuzi wa wananchi" ameeleza
Amesema kuwa Serikali chini ya Rais Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa katika Taasisi ya NIDA na sasa kasi ya uandikishaji na upatikanaji wa vitambulisho imeongezeka kwa kiwango kikubwa sana
"Jitihada hizo zimepelekea wananchi 502,790 katika Mkoa wa Songwe kupatiwa namba za utambulisho wa taifa na awamu hii tunatarajia kugawa vitambulisho 306,318 ambavyo tayari vimeandaliwa na kufika katika Mkoa wetu wa Songwe" ameeleza
Amesema kuwa katika Wilaya ya Mbozi pekee ina jumla ya vitambulisho 170,000, na mpaka sasa vitambulisho hivyo vimesambazwa kwa watendaji wa kata, mitaa na vijiji t
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa