MBOZI. Wananchi wa Wilaya ya Mbozi wametakiwa kupanda miti katika vyanzo vya maji na kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi (DAS), Tusubilege Benjamin kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Esther Mahawe wakati wa upandaji miti katika chanzo cha maji Ntosa Kijiji Cha Nambala kata ya Mlowo wilayani Mbozi ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema kuwa hayo ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo suala la mazingira ni la Muungano.
Katibu Tawala huyo amesema kuwa upandaji wa miti huo katika chanzo hicho unawakilisha zoezi hilo katika kata zote za wilaya ya Mbozi.
"Leo tunafanya hivi lakini tunawakilisha umma wa Wilaya ya Mbozi ambapo kila kata inatakiwa kufanya hiki ambacho tunakifanya kukifanya hapa" ameelekeza
"Leo tunapanda miti 2300 ambapo lengo lake ni kuweka kumbukizi ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Wilaya yetu ya Mbozi" amesema
Amesema kuwa "Miche hiyo pia ni kielelezo na ujumbe kwa wananchi wa wilaya yetu kwamba tunapaswa kutunza mazingira, kulinda vyanzo vya maji na kujenga utamaduni wa kupenda mazingira" amesema
Ameeleza kuwa miti ina msaada mkubwa katika maeneo ya watu ikiwemo kuepusha majanga hususani kipindi cha mvua kubwa na radi.
Amesema kuwa eneo likiwa wazi bila miti radi ikipiga ni rahisi madhara kuwa makubwa.
Katika zoezi hilo la upandaji miti lililofanyika leo Jumatano Aprili 19, 2023, miti 2,300 imepandwa ambapo kati ya miti hiyo 2, 200 imetolewa na TSF huku familia ya Mwaisoloka ikitoa miche100.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa