Mkuu wa mkoa wa Songwe Mhe Daniel Chongolo amewataka wakazi wa Mbozi kuhakikisha wanajenga utamaduni wa kupanda miti ili kutunza mazingira na kuacha tabia ya kupanda miti kwa matukio
Mkuu wa Mkoa huyo ameyasema hayo leo wakatia wa zoezi la upndaji miti lililofanyika leo Jumanne Aprili 23, 2024 katika eneo la Ilembo kata ya Vwawa
Mkuu wa Mkoa huyo amesemakuwa wananchi wanatakiwa kupanda miti kwa dhamira, nasio kufanya kama kazi, na inatakiwa miti ikipandwa ionekane isiwe ya kutafuta
"Nimeambiwa Halmashauri ina lengo la kupanda miti milioni 2 kwa mwaka lakini nikisema nitembee kuhesabu miti hiyo hata elfu moja sidhani kama itafika" amesema Mkuu wa Mkoa huyo na kuongeza
‘’Mimi ni seme ni lazima tuanze kuutengeneza huu utamaduni tokea shuleni, tutapita Kila shule tukute shule inakuwa na sehemu hifadhi ya msitu Shule, maeneo yetu mengi bado yana nafasi ya kuwapa wanafunzi sehemu ya kujifunza utamaduni wa kupanda miti’’ amesisitiza
Mhe. Chongolo amesemakuwa tukiwapatia shule ekari tano na kuwapa maelekezo ya kuitunza kuhakikisha miti hiyo unakuwa na pia TFS waende waweke vibao kutambulisha miti hiyo kwa kutumia majina ya asili na Kila mti na faida zake.
‘’Katika changamoto ya uvamizi nchi yetu inauongozi kuanzi ngazi ya Kijiji, kunawatu wameajiriwa na Serikali na wanalipwa mishahara, kunamtu amechaguliwa na wananchi awaongoze kwa niaba Yao kwanini eneo livamiwe nae yupo maana yake hajatimiza wajibu’’ amesema
‘’Napanga Siku ndani ya mwezi wa tano nitakuja kuzinguka na machifu, harafu waniambie mipaka iko wapi na waniambie hicho Kijiji ni Kijiji gani yule ambaye amepewa dhamana na Serikali lakini hajatimiza wajibu wake tutasalimia wakati huo tukikuta kunachangamoto’’
Hatuwezi kuwa na changamoto wakati Kuna watu wamepewa dhamana wanachukulia mambo kawaida hakuna kukaa kienyeji Kila mtu atimize wajibu wake Hilo halina haja ya maneno mengi
Machifu ninyi mmesema mnateknolojia ya ulinzi basi mi nitakuwa jaji wa hizo kesi zitakazo tokea humo msituni msipate shida iwekeni hiyo teknolojia nami nitakuwa ntakuja kuwatembelea
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa