Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Farida Mgomi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje amewataka wananchi wa kijiji Cha Isenga na Idunda kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika chanzo cha mto Isenga
Mhe. Mgomi ametoa maagizo hayo leo Jumamosi Machi 23, 2024 wakati wa uzinduzi wa shughuli ya upandaji miti katika kuhitimisha wiki ya maji ambapo zoezi hilo limefanyika katika kata ya Idiwili.
Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa "Tunapohitimisha wiki hiyo ya maji kama Wilaya wameamua kupanda katika chanzo hicho baada ya kuona umuhimu mkubwa wa chanzo hicho,
"Nataka muelewa kwamba kila mtu anadhamana katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa kwa kutofanya hivyo tunakaribisha umaskini na madhara mbalimbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi" ameeleza na kuongeza;
"Chanzo hiki cha Isenga kina umuhimu mkubwa sana kwa wananchi wa Mbozi kutokana na chanzo hicho kutegemewa na wananchi wa vijiji saba ambao wapatao 24376"
Amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 5 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji kupitia RUWASA ili kuweza kutekeleza mradi huo.
"Tunapokuwa na uhakika wa maji tunakuwa na amani na utulivu maana maji ni muhimu sana.
Tunakila sababu kuhakikisha tunatunza vyanzo vya maji na utunzaji wa mazingira maana hizi ni sera za serikali na tukumbuke pia upatikanaji wa maji unategea vyanzo vya maji.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa