Wananchi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kuhakikisha watoto chini ya umri wa miaka 8 wanapata chanjo dhidi ya ugongwa hatari wa Polio
Rai hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, John Mwaijulu akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Francis Michael katika uzinduzi wa chanjo ya ugonjwa wa polio uliofanyika eneo la Mlowo Wilaya ya Mbozi
Akitoa salamu za mkoa mwakili wa mkuu wa mkoa amesema kuwa zoezi hilo la chanjo litafanyoka kwa siku nne kuanzia leo Septemba 21 hadi Septemba 24, 2023.
"Chanjo hii ni salama kabisa itafanyika nyumba kwa nyumba, mashuleni, katika nyumba za ibada;
Natoa rai kwa wananchi wote kuepuka taarifa zozote za uzushu kuhusiana na chanjo hii" amesisitiza
Mwakilishi kutoka TAMISEMI Ally Kananika amesema kuwa wizara hiyo na Wizara ya Afya zimejipanga kuhakikisha jamii inakingwa na magonjwa yote ambayo yanazuilika kwa chanjo.
Amewasihi wananchi wote, wazazi na walezi kuhakisha watoto wote wanapata chanko.
Kwa upande wake afisa programu kutoka Wizara ya Afya, Penifored Joel ametoa rai kwa wananchi kuwa na mwamko wa kushiriki zoezi hilo na kuendelea kufuatilia chanjo kwa watoto wao hata kama isipokuwa kipindi cha kampeni kwasababu chanjo ni kinga.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa