MBOZI. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, George Musyani ametoa rai kwa wananchi wa wilaya hiyo kuchangia nguvu kazi katika miradi inayoletwa na Serekali.
Musyani ametoa rai hiyo leo Jumanne Aprili 4, 2023 wakati Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ilipotembelea ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Maninga kata ya Bara kwenye ziara ya kamati hiyo ya siku tatu ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya inayotekelezwa na Serikali.
Amesema Serikali inapeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo hivyo wananchi wanaweza kuchangia nguvu kazi ili kukamilisha miradi kwa wakati.
"Serikali inaleta fedha hizi kukamilisha miradi hii, ni nyingi kwa kuzitamka lakini ni chache katika utekelezaji. Inatakiwa huduma zipatikane hapa tuweke miundombinu ya maji kichomea taka na shimo la kondo" amesema
"Ninyi ni sehemu ya mradi na ninyi mjiongeze katika matumizi ya fedha hizo zimalize ujenzi isije ikatokea hatujakamilisha" amedokeza
Amesema kuwa wananchi wanaweza kushiriki shughuli hizo kwa kusaidia vitu ambavyo wanaweza kuvifanya kama kupeleka maji au mchanga.
"Wananchi mkileta ndoo ya maji au mchanga inahesabika imechangia, mchango sio lazima fedha" amesisitiza
Amesema kuwa zahanati ikikamilika itasaidia wananchi kupata huduma za afya kwa urahisi.
"Mheshimiwa Rais ameleta mradi huu ili kuwakomboa na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. Ipo dhana potofu kwa wananchi kuona milioni 50 ni nyingi sana msipo maliza mradi maumivu ni ya kwenu wakazi wa maeneo haya lakini ukiisha faida kwenu" amesema
Ongezeni nguvu kazi ili chenji ikibaki muanze ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa zahanati ili hata kama kuna mgonjwa usiku unamwamsha ili akuhudumie kuliko akikaa mbali
Amesema kuwa zahanati hiyo ikikamilika itawahudumia wakazi zaidi 4600 ambao kwa sasa wanafuata huduma hizo katika vijiji jirani na Kijiji hicho.
Kamati hiyo ipo kwenywe ziara ya siku tatu ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ambapo kwa leo kamati ikiwa kwenye siku ya pili ya ziara imetembelea ujenzi wa nyumba ya mwalimu Usunje kata ya Isansa, jengo la zahanati Kijiji cha Maninga kata ya Bara, ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Ilalangulu kata ya Nambinzo na ujenzi wa bweni sekondari ya Naiputa kata ya Nambinzo.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa