Walimu wa shule za msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wametakiwa kufuata kanuni bora za ufundishaji kwasababu ni watu wanaotoa mwelekeo, ujuzi na ufahamu kwa wanafunzi
Hayo yamesemwa leo Alhamisi 14, 2024 na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bi. Dorothy Mwandila wakati wa kikao kazi na walimu wa shule za msingi katika kata ya Mlowo
Akizungumza na walimu hao afisa elimu huyo amesema kuwa, walimu wana jukumu kubwa la kufundisha na wao wanatoa mwelekeo, ujuzi na uhfahamu unaohitajika kwa maendeleo ya kielimu kijamii na kiakili.
"Walimu mnawezakuwa na athari kubwa kwa maisha ya wanafunzi na uwezo wa kuhamasisha kuongoza na kuwa mfano bora
Walimu wengi wanawaachia wanafunzi kuandika kazi kwa wenzao madarasani kituo ambacho sio sawa katika kupandisha taalumu" amesema
Serikali ina imani kubwa sana na ninyi walimu ndio maana mnapewa fedha za likizo, mmenunuliwa vishikwambi ukilinganisha na kada zingine, kwanini hatufundishi tumepatwa na nini
Katika kikao hicho mambo mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo taaluma, usimamizi wa miradi, usimamizi wa fedha za ruzuku, kufahamiana na kujua changamoto za walimu
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa