Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Esther Mahawe amewataka wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanatoa risiti za kielekroniki wanapouza bidhaa katika maduka yao.
DC Mahawe ametoa wito huo leo Alhamisi Oktoba 20, 2023 wakati wa zoezi la ubandikaji stika za TRA katika maduka ya wafanyabiashara katika mji mdogo wa Mlowo.
Katika zoezi hilo Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa muuzaji ana wajibu wa kutoa risiti na mnunuaji bidhaa anatakiwa adai risiti.
"Unaponunua bidhaa mbalimbali katika maduka kumbuka kudai risiti na unapomuuzia mteja hakikiksha unampa risiti" amesisitiza
Mhe. Mahawe amesema kuwa kodi hizo zinapokusanywa ndizo zinasaidia kupata maendeleo katika maeneo husika ambapo Serikali inategemea kodi hizo ili ipate fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na huduma.
"Hizi fedha tunazozikusanya kupitia mashine za EFD ndizo zinaleta zahanati, vituo vya afya, barabara, maji nk. Niendelee kuwatia shime wana Mbozi unaponunua kitu chochote dai risiti, ili tuweze kujenga Tanzania moja maana ndio pekee tuliyonayo tutaijenga kwa nguvu zetu" amesema DC Mahawe na kuongeza;
"Nitoe wito kwa TRA muwe mnapita mara kwa mara katika maduka ya wafanyabiashara ili kuona kama haya yanatekelezwa kwa vitendo. Niseme tu tuko pamoja na tunamsapoto Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazoendelea kuzifanya. Na tumeona mapato yanavyozidi kupanda na kila mahali katika nchiameeleza"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa