• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

WADAU WAOMBWA KUCHANGIA WANAFUNZI WALIOJIUNGA SHULE BILA VIFAA, SONGWE

Kurushwa hewani: February 18th, 2023

MBOZI.Wadau mbalimbali mkoani Songwe wameombwa kujitokeza kusaidia michango na vifaa ili kuwawezesha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ambao hawana vifaa na sare katika mkoa huo.


Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Februari 18, 2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe (RAS), Happiness Seneda  wakati wa mazoezi ya kujenga afya maarufu 'Back to School Songwe Jogging Club' yenye lengo la kuhamasisha wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni kujiunga na masomo.


Katika mazoezi hayo ambayo yameongozwa Katibu Tawala huyo wa mkoa  yaliambatana na kukabidhi vifaa baadhi ya wanafunzi ambavyo vimetolewa na wadau mbalimbali.

Katibu Tawala huyo amesema kuwa vifaa hivyo vimechangiwa na wadau wakiwemo Tanroads ambao wamechangia vifaa vyenye thamani ya Sh300,000, Mbunge wa Jimbo la Mbozi, George Mwenisongole akichangia vifaa vyenye thamani ya Sh50,000 huku Shirika la Tanzania Communication and Development Centre (TCDC) likichangia madaftari kwa wanafunzi 17 huku akitoa rai kwa wadau wengine kuchangia.


RAS huyo ambaye ni mhamasishaji mkuu na mshiriki wa mazoezi hayo ya kujenga afya ya mwili amesema kuwa michango inayotolewa inasaidia wanafunzi amabo wameripoti shuleni bila vifaa.


"Nawaomba wadau kutoa michango mbalimbali ya vifaa vya shule ili tuwasaidie watoto wetu waende shule" amesema RAS Seneda


Pia, amewashukuru waliojitokeza kushiriki kwenye jogging hiyo akisema kuwa Jumamosi ijayo itakuwa wilayani Songwe.


"Mazoezi ni afya hatutaki vitambi fanya mazoezi kila siku ila Jumamosi ni ujuzi tu kuoneshana, Tunawashukuru sana waliochangia vifaa" amesema na kuongeza


"Mazoezi tunayoyafanya yana impact, kidato cha kwanza asilimia zimefika 86 na awali asilimia 97 tunafanya kampeni hii ili asilimia hiyo iliyobaki iende shule"


Amesema kuwa programu hiyo ambayo inakwenda kwenye wilaya zote za Mkoa wa Songwe ilianzishwa ili kuwahamasisha watoto ambao hawajajiunga na shule wajiunge hata kama hawana vifaa wala sare ambapo anatapokelewa  aendelee na masomo huku wadau wanamchangia akiwa shuleni.


"Wiki ijayo tutakuwa Songwe" amesisitiza Katibu Tawala hiyo wa Mkoa wa Songwe.


Wanafunzi waliopewa vifaa ni pamoja na Jestina Manipembe wa shule ya Sekondari Nkanga, Flora Kashililika shule ya  Shaji, Lena Ndidi wa Hezya Sekondari na Enelisa Mgala kutoka shule ya Sekondari Bara.


Jumala ya Wanafunzi wahitaji ni 300 kimkoa lakini wanaopata kimkoa 50 huku kwa wilaya ya Mbozi vifaa  vimetolewa kwa wanafunzi 10.


Jogging hiyo ambayo hufanyika kila Jumamosi ni moja ya mkakati wa mkoa wa Songwe wenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza ambao hawajajiunga na masomo waripoti shuleni hata kama hawana vifaa

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa