Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega ametaka wanawake ambao ni watu wazima maarufu (mashangazi ) wenye tabia ya kujihusisha kimapenzi na vijana wadogo kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume na maadili na husababisha kuibuka wimbi la vijana wa kiume kutokufanya kazi wakitegemea kulelewa na wanawake waliowazidi umri.
DC Mbega ametoa ushauri huo leo Ijumaa Machi 7, 2025 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani 2025 ambayo kiwilaya yamefanyika katika Kata ya Idiwili wilaya ya Mbozi.
Mbega amesema kuwa tabia hiyo inawafajya vijana wengi wa kiume kuwa wavivu na kukaa bila kujishughulisha wakiamini kuwa watapata wa kuwalea.
Lakini katika hatua nyingine amesema s vijana wengi wanaogopa gharama kwa mabinti hali inayo pelekea baadhi Yao kuwakimbilia wanawake walio wazidi umri
Pia, DC Mbega amewashauri wanawake walioachana na waume zao kutopandikiza chuki kwa watoto wao kujenga chuki kwa baba zao .
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa