• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

TAKUKURU YATAKA UTEKELEZAJI MIRADI KWA WELEDI NA WAKATI, SONGWE

Kurushwa hewani: February 21st, 2023

MBOZI. Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuaia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Songwe, Mohamed Shariff ametoa wito kwa wote wenye dhamana ya kutekeleza, kufuatilia na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali mkoani humo kuhakikisha inatekelezwa kwa weledi na kwa wakati.


Shariff ametoa wito huo leo Jumanne 21 Februari 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Takukuru mkoa wa Songwe.


Amesema kuwa katika kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali yanayohusu rushwa Ofisi za Serikali za Mitaa ndio zinalalamikiwa zaidi ikifiatia elimu, polisi na kilimo.


Shariff ametaja sababu ya sekta ya Serikali za Mitaa kulalamikiwa zaidi ni kutokana na sekta hiyo kukutana na wananchi moja kwa moja ambapo kunakuwa na usumbufu, kutokuwepo maeneo ya kazi pamoja  akutopokea simu.


"Serikali za Mitaa wanadeal na watu moja kwa moja endapo wasipotimiza wajibu wao ndio maana malalamiko yanakiwa mengi zaidi" amesema


"Niwaombe wanahabari kuendelea kuelimisha na kuuhabarisha umma ili jamii izidi kutambua wajibu wao katika kufichua vitendo viovu vyenye viashiria vya rushwa katika zoezi hili muhimu Kwa ustawi wa jamii" amesisitiza


Ametaja mkakati wa kwanza wa Taasisi hiyo wa kutokomeza rushwa kuwa ni kutoa elimu kupitia Takukuru _Rafiki ambayo itaongeza wigo wa kushirikisha wananchi na wadau katika kutambua na kutatua kero katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo zinazoweza kuisababisha kutolea vitendo vya rushwa.


Pia, Shariff amebainisha kuwa Takukuru imejipanga kufanya uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa mageti ya maliasili, mfumo wa usambazaji  mbolea za ruzuku, kufanya ufuatiliaji wa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri zinazopelekwa kwenye miradi, na asilimia 10.


Ameeleza kuwa kuwa katika kipindi cha robo ya pili taasisi hiyo imefanya ufuatiliaji wa miradi 68 yenye thamani ya Sh11.5 bilioni inayotekelezwa katika sekta ya afya, elimu, miundombinu, maji na mifugo


Ameongeza kuwa miradi iliyobainika kuwa na mapungufu hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na wahusika kuelekezwa kufanya marekebisho, kuongeza ufuatiliaji, kutunza vizuri nyaraka, kuongeza kasi ya ujenzi, kuwashauri wakurugenzi kuangalia namna ya kumalizia miradi kupitia vikao vya maamuzi.


 Katika uchambuzi wa mfumo wa masoko taasisi hiyo imeshauri asilimia 20 ya mapato yanayokusanywa yarejeshwe ili masoko yaweze kujiendesha.


Pia, amesema Takukuru imeshauri halmashauri iteue au kuajiri maofisa masoko au mameneja ili waweze kusimamia uendeshaji wa masoko kama vile usafi, ulinzi, pamoja na uboreshaji wa moundombinu ya masoko hayo.


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa