SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema amekuja kuboresha yale yote mazuri ambayo yamefanyika na watangulizi wake.
Dk Michael aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo Februari 26 mwaka huu kushika nafasi ya Waziri Kindamba ambaye amehamishiwa mkoani Tanga.
Dk Michael anakuwa mkuu wa mkoa huo wa awamu ya tano tangu uanzishwe mwaka 2016, ambapo mkuu wa mkoa wa kwanza alikuwa Chiku
Galawa akafuatiwa na Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela, Omary Mgumba na Waziri Kindamba.
Leo Ijumaa Machi 3, 2023, Dkt. Francis Michael wakati akizungunza na watumishi wa Ofisi ya Mkoa kwa lengo la kufamiana na kuweka mikakati ya kazi ili kufikia lengo la Rais Samia la kuwaletea maendeleo wananchi wa Songwe, ameahidi kuyaendeleza mazuri ya watangulizi wake.
Amesema mikakati yote iliyowekwa ya maendeleo kwa wananchi wa Songwe itaendelezwa kwa kushirikiana na watumishi pamoja na wananchi.
"Katibu Tawala wa Mkoa ondoa hofu sitabadilisha jambo zuri ambalo mmelifanya nitajifunza mengi kutoka kwenu naomba ushirikiano wenu tutaboresha mikakati yote iliyofanyika na mtangulizi wangu" amesisitiza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amesema watumishi wote wa Songwe wako tayari kutoa ushirikiano na kutekeleza maelekezo yote yatakayotolewa na Mkuu wa Mkoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Mhe. Methew Chikoti akiongea kwa niaba ya madiwani wa Mkoa wa Songwe amempongeza Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael kwa kuaminiwa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza Songwe na kuhaidi kutoa ushirikiano wa kutosha.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amesema watahakikisha wanaboresha ushirikiano na kuimarisha ili waweze kuleta maendeleo kwa wananchi.
Wakati huo huo, Mhe. Dkt. Francis Michael amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuja kufanya kazi Songwe
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa