• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

RC Kindamba: Tutoke enzi za kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku, songwe

Kurushwa hewani: January 2nd, 2023

Songwe.Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia elimu waliyoipata wakati wa maadhimisho ya wiki ya Sheria iwasaidie kupata suluhu ya migogoro katika jamii huku akiwaasa kutoka zama za kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku.

RC Kindamba ametoa rai hiyo leo Jumatano Februari mosi, 2023 wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Songwe iliopo Nselewa.

Tutoke katika enzi za kuuza ng'ombe Kwa kesi ya kuku, lazima tutafute Suluhu ya migogoro yetu

Amesema kuwa kupitia maadhimisho hayo wadau wa mahakama watawaongoza wadaawa ambao ni mshtaki na mshtakiwa katika kutatua mgogoro wao kwa njia ya usuluhishi.

"Ni matumaini yangu watu wa mahakama na wananchi wa Mkoa wa Songwe wameyatendea haki maadhimisho ya wiki ya Sheria mpaka kufikia leo kilelele cha maadhimisho hayo kwa kujitokeza kupata elimu na kufahamu hatua mbalimbali za kufungua majalada mahakamani" amesema mkuu huyo wa mkoa.

Katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu: wajibu wa mahakama, RC Kindamba ametoa wito kwa jamii kutafuta njia bora za utatuzi wa migogoro na si kuendeleza zilizopitwa na wakati.

"Tutoke katika enzi za kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku, lazima tutafute suluhu ya migogoro yetu" amesesitiza mkuu huyo wa mkoa na kuongeza;

"Mkoa wetu sio kisiwa tumeshuhudia mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) ameruhusu mikutano ya kidemokrasia kutafuta suluhu ya migongano mbalimbali ili kulinda haki na usawa katika jamii" amesema

Ameeleza kuwa Rais Samia anatamani watanzania wote wanapata haki maana  haki ni msumeno inakata mbele na nyuma hata vitabu vya dini vimeandika.

"Mahakama imekuja na hili kwani suluhu huleta mahusiano mazuri kuliko kupekekana mahakamani kumaliza muda, pesa husababisha kutopata mahusiano mazuri" amesema

Amewataka waliopewa zamana ya kuwasimamia wananchi watende haki.

Akisoma hotuba yake kwa mgeni rasmi Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Hassan Makube amesema kuwa mahakama inajukumu la kuhakikisha kuwa suala la utoaji haki linafanyika kwa wakati ili kuwezesha wananchi kufanya shughuli zao za kimaendeleo

Amezitaja faida za kutatua migogoro  kuwa ni pamoja na upatikanaji wa haki kwa wakati kwani hakutakuwa na matumizi mengi ya taratibu za kisheria

"Pia hupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani, watu watapata muda mwingi wa kufanya shughuli za maendeleo" amesema

"Vilevile itasaidia kuimarisha amani na ustawi wa jamii kwasababu italinda uhusiana wa wadaawa hasa pale kunapokuwa na mgogoro" ameeleza Makube

Makube amezitaja changamoto za kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kuwa ni uelewa mdogo wa njia hii, kutokuwa tayari kujishihusha na gharama ya kuwalipa wasuluhishi nje ya mahakama.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba, Fakii Lulandala ambaye amekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amesema kuwa katika moja ya jukumu la ofisi ya mkuu wa wilaya ni usuluhishi wa migogoro hivyo ofisi hiyo ninapunguza kesi mahakamani

"Sisi ni miongoni mwa wahusika tunatamani kuona mahakama inafanya kazi kwa ufanisi na maridhiano" ameswma DC huyo

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa