Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Daniel Chongolo amekagua zoezi la maboresho ya miundombinu na uunganishwaji wa vyumba vya biashara na pia kuagiza wajasiriamali wote kuanza biashara zao ndani ya stendi ya mabasi Mlowo
Hatua hiyo imekuja baada ya vibanda hivyo vilivyojengwa hapo awali kuwa ni vidogo ambapo Mhe. Chongolo aliagiza vibanda hivyo kurekebishwa kwa kuunganisha vyumba viwili kuwa kimoja.
Mkuu wa Mkoa huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kuuza biashara zao kuongeza kipato
‘’Kituo chetu hiki kiwe senta ya mauzo au biashara cha mkoa kwahiyo wananchi watumie hii fursa kama hatupo tayari watakuja walio tayari’’ amesema
Ameahidi kuwa atarudi tena katika stendi hiyo ili kuona mchakato unaendeleaje na kuangalia mpangilio wa mabasi na wajasiliamali unaendaje.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa