Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Daniel Chongolo ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kufanya maboresho ya miundombinu katika stendi ya Mji Mdogo wa Mlowo ili ianze kutumika tena.
Mhe. Chongolo ametoa maagizo hayo leo Jummanne Mei 14, 2024 wakati wa mkutano na wamiliki wa vyumba vya biashara katika stendi hiyo.
Katika Mkutano huo makubaliano na wafanyabiashara hao yaliofikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kurudi ndani ya stendi ya mabasi pamoja na mabasi kuingia ndani ya stendi.
Pia vyumba vya biashara vyote vya mbele kuunganishwa kutokana na udogo wa vyumba hivyo ambapo vyumba viwili vitatoa chumba kimoja.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa Siku ya Ijumaa atashiriki kikao kitakachohusu uunganishaji wa vyumba hivyo.
Hata hivyo, RC Chongolo amepiga marufuku ujenzi holela ambao haufuati taratibu za mipango miji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa