Mkuu wa Mkoa wa Sojgwe, Mhe. Daniel Chongolo amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Karasha ambayo imejengwa kupitia mradi wa Sequip awamu ya pili.
Mhe. Chongolo ametoa pongezi hizo leo Alhamisi Februari 13, 2025 wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Akizungumzia miradi aliyoitembelea na kuikagua, Mhe. Chongolo ameitaja shule hiyo ya sekondari ya Sequip awamu ya pili kuwa imejengwa kwa viwango.
"Mimi nimetembea kwenye majengo mengi ya shule lakini ukiangalia kwa shule hii imejengwa vizuri sana. Kuna changamoto za kawaida sana ambazo ni chache za kurekebisha lakini hongereni sana" amesema
Mkuu wa Mkoa huyo ameahidi kupeleka shule nyingine katika kata hiyo ya Mlowo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma kwa shule hizo zilizopo
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo ametoa wito kwa wenyeviti wa Kijiji na vitongoji kuhakikisha wanafunzi waliopangiwa shule wanaripoti shuleni kabla sheria haijaanza kuchukua mkondo wake.
Pia, katika ziara hiyo, Mhe. Chongolo amemkabidhi mradi kwa mkandarasi kwajili ya uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji, kuona usambazaji wa umeme katika kitongoji cha Ilonga Kata ya Mahenje, kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Shule mpya ya Sekondari Karasha, kukagua na kuona miundombinu ya afya Hospitali ya Vwawa, kukagua upanuzi wa mradi wa maji Vwawa-Mlowo na shule mpya ya Sekondari Sakamwela mradi wa Sequip kata ya Mlowo.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa