Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi Happiness Seneda amewataka wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kusikiliza na kutatua kero za watumishi wa Wilaya hiyo.
Amesema hayo leo Jumanne, Oktoba 24, 2023 watikati wa ziara ya kukagua na kufanya tathimini ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo.
Akizungumza na watumishi wa Tarafa ya Iyula, Katibu Tawala huyo amesema kuwa ukiwasikiliza watumishi vizuri watatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
"Hebu wasikilizeni watumishi kero walizonazo na kuzitatua ili wafanyekazi kwa bidii" amesema
Amesema kuwa bila kutatua kero za watumishi wanakuwa na mawazo mpaka wanapata magonjwa yasio ambukiza ikiwemo presha, kisukari na vidonda vya tumbo.
Hata hivyo Bi Seneda ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo.
"Tumekuta katika miradi kuna ushirikishwaji mzuri wa wananchi na viongozi kuanzia ngazi ya chini,
"Niongeze kuwapongeza sana Halmashauri ni vigumu kukuta mradi umekamilika na fedha zikabaki hii ni mara chache sana ninawapongeza" amesema
"Nimefurahishwa sana na usimamizi wa mradi wa BOOST shule ya msingi Idunda ambao walipokea milioni 106 ujenzi wa madarasa 4 na matundu 3 ya vyoo lakini wamebakiza chenji kama milioni 5,600,000"
"Maeneo mengi ya miradi unakuta yamekamilika lakini wanakwambia bajeti haikutosha tuongeze hiki mara kile" amesema
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa