Polisi Mkoani Songwe wametakiwa kuzingatia kanuni na taratibu wakati wanatimiza wajibu wao.
Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Januari 27, 2024 na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Gallus Hyera wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi (Police Family Day) yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Vwawa wilayani Mbozi.
Amewataka kusimamia kiapo chao cha kuitumikia jamii kwa kuwalinda wananchi na mali zao.
Akizungumzia Siku hiyo maalumu, Hyera amesema kuwa familia zao zimekuwa nguzo kubwa katika kuwasaidia polisi hao kuondokana na msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa kazi wanayoifanya.
"Lengo ni kujenga jukwaa la kuimarisha uhusiano na kuonesha shukrani kwa familia ambazo zinaunga mkono na kuhimiza polisi wakati wa kutimiza majukumu na wajibu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na miongozo" ameeleza
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa