Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu , Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali inaweka mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavuna waweze kupata haki ya elimu ili wapate ujuzi.
Profesa Ndalichako amebainisha hayo leo Jumanne Agosti 23, 2023 wakati alipotembelea ujenzi wa chuo cha watu wenye ulemavu kinachojengwa katika eneo la Ukwile wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Amesema kuwa Serikali imejikita kuhakikisha inatoa elimu inayompa mtu ujuzi ambapo mtu akitoka anaweza kujiajiri au akaajiriwa.
"Serikali ya awamu ya sita imeona ni vizuri kutengeneza vyuo ambavyo vitakuwa vinaweza kutoa mafunzo na marekebisho" amesema
Amesema kuwa Rais Samia anasisitiza watu wenye ulemavu wapate fursa sawa na watu wengine.
"Mheshimiwa Rais ametoka Sh3 bilioni kuanzia katika mwaka wafedha 22/2023 ambazo fedha hizo zilipokelewa mwezi wa nne na tunajenga vyuo vitatu katika Mkoa wa Songwe, Ruvuma pamoja na Kigoma".
Amesema kuwa anamshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa kutoa eneo bure la ujenzi wa chuo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe dkt Francis Michael ameomba kupitia Wizara kurekebisha ramani za nyumba za watumishi kwani za sasa ni ndogo
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa