Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Daniel Mushi amefungua rasmi mafunzo rejea kwa maafisa ugani wa mifugo wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini iliyohusisha mikoa ya Songwe,Rukwa, Katavi, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Iringa.
Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Jumatatu 25 Machi 2024, katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Nselewa, Mbozi.
Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu katibu mkuu huyo amesema kuwa sekta ya mifugo haijawahi kupata kipaumbele kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita hivyo wana kila sababu ya kutumia fursa hiyo ilikuleta mabadiliko chanya kwa wafugaji
‘’Sisi kama Wizara tunawajibu wa kutengeneza sera na miongozo na wanaokwenda kutafsiri hiyo miongozo ni ninyi maafisa ugani, sisi tunawaona kama kiungo muhimu sana katika kuleta chachu ya mabadiliko katika sekta katika sekta ya kiuchumi’’ amesisitiza na kuongeza;
‘’Ndio maana Tukasema hebu tukutane leo tujengeane uelewa wa pamoja tuweze kukumbushana mambo machache kwa hiyo haya mafunzo ni muhimu sana, nisisitize kwamba mafunzo hayo mtakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo na tusipo yatendea kazi ni kazi bure’’.
Profesa Mushi amesema kuwa Tanzania inasifa kubwa ya kuwa nchi ya pili Barani Afrika kuwa na mifugo mingi ukiachana na Ethiopia
Vile vile Naibu katibu mkuu huyo amese makuwa kanda ya Nyanda za Juu kusini maarufu kwa ng’ombe wa maziwa hivyo wizara ina kila sababu ya kuwekeza zaidi ili tija ipatikane kwa ngombe hao wa maziwa
‘’Na pia tunakwenda kuanzisha kituo kipya cha mafunzo ya mifugo ngazi ya Cheti hapa Mkoa wa Songwe ambacho kitajengwa Wilaya ya Mbozi katika kata ya Igamba Kijiji cha Mbozi ambapo mkandarasi ameshapewa mkataba wa kuanza kazi.
Akizungumza katiaka mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Farida Mgomi amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa kupata fursa ya kupata mafunzo.
‘’Sekta ya mifugo ni imepiga hatua sana kwa kiasi kikubwa sana, wengi wetu tumeshawahi kushuhudia maafisa ugani wakipewa pikipiki ilikuwawezesha kuwafikia wafugaji katika maeneo
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa