MUSYANI: MADIWANI TUJITAHIDI KUJUA KINACHOENDELEA KWENYE TAASISI ZETUMBOZI:
Kurushwa hewani: June 7th, 2021
MUSYANI: MADIWANI TUJITAHIDI KUJUA KINACHOENDELEA KWENYE TAASISI ZETUMBOZI: Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mhe. George Musyani ametoa wito kwa waheshimiwa Madiwani wa Mbozi kuwa na utaratibu wa mara kwa mara kufuatilia Taasisi zilizopo kwenye Kata zao ili wajue mambo yanayoendelea."Kwa sasa Serikali inaleta fedha za maendeleo moja kwa moja kwenye Taasisi zetu, nyingine zinapitia hapa Halmashauri sasa Diwani ukisubiria hadi vikao ndio ujue kuna kitu gani haipendezi" George Musyani.Mhe. Musyani amesema ukikuta kuna fedha imeingia kwenye Taasisi yako mara moja anza kufuatilia utekelezaji wake ili utekelezaji wake ufanyike kwa wakati.Mwenyekiti ametoa wito huo wakati wa mafunzo Maalumu ya Madiwani kuhusu usafi wa mazingira ambao unaendeshwa na Mkoa kwa ufadhili wa UNICEF wenye lengo ifikapo 2023 kaya na Taasisi zote kuwa vyoo bora.