Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amemwapisha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamadi Rajabu Mbega huku akimpa maagizo matano yanayohitaji msukumo.
Mhe. Chongolo amemwapisha Mkuu huyo wa wilaya mpya ya Mbozi leo Jumatano Januari 29, 2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Nselewa Wilayani Mbozi.
Akizungumza wakati wa Hafla hiyo, Mhe. Chongolo amemtaka mkuu wa wilaya huyo kutoa ushirikiano kwa viongozo ngazi zote atakaowakuta.
"Nikuombe utakapokabidhiwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kashirikiane na viongozi utakaowakuta kwenye ngazi zote katika kutatuachangamoto ambazo zitafika Ofisini kwako, kwani changamoto za Wananchi ndio hasa dhamana tulioyopewa kuitumikia kwayo. Nikuombe kwenye eneo hili ukatatue changamoto za wananchi kwa uaminifu na uadilifu kwani wananchi wana imani kubwa na Serikali hii" amesema
Pia, RC Chongolo amempa maagizo matano ambayo yanahitaji msukumo yakiwemo, Kutokomeza Mimba za utotoni sambamba na mdondoko wa wanafunzi mashuleni, Kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora, Kuendeleza jitihada za afua za Lishe kupunguza udumavu, Kuhamashisha maendeleo ya wananchi pamoja na Kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa ubakaji, ulawiti na mauaji
ya wananchi.
Mhe. Hamadi Rajabu Mbega aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua nafasi ya Mhe. Ester Mahawe ambaye alifariki dunia Januari 14, 2025
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa