Wataalamu wa Idara ya Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wamefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kwa lengo la kubadilishana uzaoefu wa utendaji kazi ili kuboresha sekta ya elimu.
Ziara hiyo ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe. George Musyani ikiwahusisha watendaji wa Idara ya Elimu Awali na Msingi pamoja na waratibu elimu kata wa kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imefanyika leo Ijumaa Aprili 12, 2024 katika Halmashauri ya Nachingea mkoani Lindi.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe. George Musyani amesemakuwa kupitia ziara hiyo wamejifunza mikakati mbalimbali inayopandisha kiwango cha elimu.
"Tumeona walimu walivyo na ushirikiano na wazazi, tumeona utolewaji wa chakula mashuleni kamati zinavyokusanya vyakula na kuleta shuleni kwaajili ya wanafunzi;
Kingine tumejifinza uwazi wa walimu wakuu kwa staff wenzao katika matumizi ya fedha za capitation. Tumefungua dirisha hili la undugu tunaomba ushirikiano wenu" amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Adinan Mpyagila amesema kuwa wamewekeza hasa kupitia mazao ikiwemo uuzaji wa zao la korosha katika kuboresha sekta ya elimu.
"Sisi nachingwea tumewekeza kweli kweli, kwa msimu huu wa korosho tumeweka zaidi ya shilingi milioni 500 kwaajili ya uboreshaji wa elimu ili kuhakikisha tunafanya vizuri ndio maana matokeo yanakuwa mazuri
"Naamini mmejifunza mengi na mtakwenda kuyapeleka katika Halmashauri yenu" ameeleza
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa