Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023, Abdalla Shaibu Kaim amesema kuwa Wilaya ya Mbozi imewafurahisha kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali akieleza kuwa Wilaya hiyo imemtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema hayo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 baada ya kuhitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo amesema kuwa Wilaya hiyo imefunika kwa utekelezaji wa miradi iliyotembelewa na Mwenge.
“Tumepitia miradi yote. Mbozi mmefunika sana na mmemtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji miradi kwa viwango” amesema.
Pia, Kiongozi huyo wa Mwenge amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbozi kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa miradi pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya umetupa heshima kubwa sana narudia kuesema Mbozi mmefunika na hongereni sana” amesisitiza
Amewaagiza viongozi wa Wilaya hiyo hasa wanaohusika na miradi iliyopitiwa na Mwenge kufuata ushauri waliopewa ili kuboresha zaidi miradi katika wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mh Esther Mahawe ameeleza kuwa miradi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano walionao kama Wilaya.
Amesema kuwa Mwenge huo umepitia miradi nane yenye thamani ya Sh8.2 bilioni ikiwemo miradi ya shule, zahanati, maji, excavator na kiwanda cha kufyatulia matofali.
“Tunashukuru sana miradi yetu yote imezinduliwa. Mafanikio haya yanatokana na ushirikiano tulionao katika wilaya yetu” amesema Mh Mahawe.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa