MBOZI. Baraza la Madiwani Wilaya ya Mbozi limelaani vikali vitendo vya kikatili vinavyoendelea katika jamii.
Baraza hilo ambalo limekutana leo Ijumaa Aprili 28, 2023 lilikuwa likijadili taarifa ya robo ya tatu kuanzia Januari mpaka Machi
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, George Musyani amesema kuwa kuna haja ya jamii ya watu wa Mbozi kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya hiyo kufuatilia katika vitendo hivyo na kutoa taarifa katika vyombo husika.
Mwenyekiti huyo amesema Wanambozi kuna haja ya kuondoa dhana ya kuwalinda watu wanaofanya ukatili.
Hoja hiyo imeibuka katika kikao hicho kutokana na kuwepo kwa tuhuma za mwalimu wa shule ya msingi Senjele anayedaiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita na kutoroka.
Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Vwawa, Aida Sanatu ameomba walimu kuwa walezi wa wanafunzi na sio kugeuka mwiba.
"Naomba hatua zichukuliwe haraka sisi kama madiwani tunalaani vikali vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia"
Diwani wa Kata ya Igamba .... amesema "Watoto wetu wataziona taasisi zetu kama jehanamu tuna jambo la kufanya kuwarudisha walimu katika suala ya uadilifu" amesema
Neema Nzowa ambaye ni diwani wa viti maalum Kata ya Vwawa amesema kuwa UWT ilifanya ziara katika ofisi ya dawati la jinsia walibaini kuwa kuna hali mbaya katika wilaya ya Mbozi kutokana na kukithiri kwa matukio ya ubakaji na ulawiti
"Tunaomba ofisi ya Mkuu wa Wilaya yetu achukue hatua sitahiki na ikiwezekama waliofanya vitendo hivi hatuwataki katika wilaya yetu"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa