MBOZI. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amesemakuwa wilaya ya hiyo inakwenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo baada ya maafisa ugani kukabidhiwa pikipiki na Serikali.
Amebainisha hayo jana Ijumaa Machi 10, 2023 wakati akikabidhi pikipiki hizo 81 kwa maafisa ugani wa wilaya hiyo.
DC Mahawe amesema anaamini kama wilaya na mkoa kwa ujumla inakwenda kuzalisha kwa wingi kutokana na wataalamu wa kilimo kuwezeshwa vitendea kazi ambavyo vitawafanya wamfikie mpaka mkulima wa chini.
Akizungumza na maofisa ugani katika hafla hiyo mkuu huyo wa wilaya amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia vyombo hivyo ambavyo vitakwenda kuinua utendaji wa maofisa hao.
"Hata kama watu wanasema hawajaona kama vitu vinafanyika, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni mama anaupiga mwingi mpaka unamwagika" amesema
Tumeona kwa macho yetu juhudi za mama kwaajili ya kuwezeshwa kilimo cha kisasa chini ya Waziri wake wa kilimo Bashe.
Sitegemei vyombo hivi mkafanyie bodaboda au kufanya uhalifu wowote nategemea vyombo hivi kwenda kufanya kazi iliyokusudiwa" ameagiza
"Niwahimize muende mkafanye kazi ndugu zangu mkaoneshe kabla ya kupata pikipiki ilikuaje na baada ya kupata imekuaje" amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Gorge Musyani amesema kuwa hilo ni jambo kubwa kwani maofisa ugani walikua wamesahaulika na hivyo pikipiki hizo zimejibu kilio chao cha muda mrefu.
"Ni imani yangu kazi inayokwenda kufanyika ni kubwa itakuwa na matokeo makubwa mara mbili ya yaliyo kuwepo" amesema Musyani
"Mbozi tumebeba Mkoa wa Songwe naamini tukipanda katika uzalishaji tutaupandisha mkoa na kutoka kwenye nafasi ya tatu mpaka ya kwanza;
Rai yangu kwenu vyombo hivi viende kufanya kazi iliyokusudiwa twende tukahudumie wakulima kule chini tukatoe ushauri katika ngazi za vitongoji" amesema
"Zamani walionekana sana maofisa mifugo sio maafisa ugani sasa tukawaelimishe wakulima mazao mazuri yanapatokana kwa kufuata kanuni bora za kilimo tumuunge mkono Rais wetu kwakuleta matokeo chanya" amesema
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa