Maafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi wamehudhuria mafunzo ya siku tano kuhusu mpango wa ajira za muda ili kuziwezesha jamii kuibua miradi itakayotatua changamoto zao.
Mpango wa utekelezaji wa miradi ya ajira ya muda inayoibuliwa na jamii katika vijiji na mitaa ambapo utekelezaji wake unafanywa na kaya za wanufaika wa TASAF waliosajiliwa katika mpango wenye umri wa miaka 18 mpaka 65
Miradi ya ajira za muda ina malengo makuu matatu ikiwa ni pamoja kuongeza kipato kwa kaya za wanufaika kupitia ujira wanaopata wakati wa utekelezaji wa miradi
Utekelezaji wa miradi hiyo inatoa ujuzi kwa kaya za wanufaika kipindi wanaposhiriki katika kazi jamii kupata miundombinu ambayo inatumika kutatua changamoto iliyokuwepo awali katika eneo hilo
Utekelezaji wa miradi hiyo inaanza kipindi cha hari (kipindi ambacho mnufaika ameishiwa fedha) ambapo mnufaika anahitaji kununua pembejeo
Miradi hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Septemba mpaka Feburuari
Miradi ya ajira za muda (PWP) ni afua moja wapo inayotekeleza na mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia TASAF
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa