MBOZI. Kampuni ya One Acre Fund imetoa miche 2,800 kwa ajili ya kuhamasisha kampeni ya upandaji wa miti katika halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.
Miche hiyo ambayo imekabidhiwa leo Jumanne Aprili 11, 2023 na mratibu wa miti kampuni ya One Acre Fund, Agustino Waduma ina lengo la kusaidia uhamasishaji upandaji miti katika halmashauri za mkoa wa Songwe.
Katika hafla hiyo Waduma amezitaka halmashauri za mkoa huo kushiriki zoezi la utunzaji mazingira ili kukabiliana na ongezeko la joto duniani
Waduma ameongeza kuwa moja ya shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ni pamoja na kuwapatia wakulima miche ili kutunza mazingira, kupata matunda na kujipatia kipato.
Ametoa wito kwa jamii kuchukulia suala la utunzaji wa mazingira kuwa suala lao na muhimu na sio kuwaachia viongozi.
Mratibu huyo wa Idara ya miti wa One Acre Fund ameishukuru Halmashauri na mkoa kwa ushirikiano wanaotoa kwa kampuni hiyo
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde, Afisa Maliasili na Mazingira, Hamis Nzunda ameishukuru kampuni hiyo kwa kutekeleza kampeni ya upandaji miti kwa vitendo kwa utoaji wa miche hiyo.
Nzunda amesema miche hiyo imegawiwa katika shule za sekondari nne na shule za msingi tano.
Nzunda ametoa wito kwa jamii kutekeleza kampeni ya upandaji miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya kutunza mazingira, matunda, nishati na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa