MBOZI. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbozi, Majaliwa Mlawizi amesema kazi ya chama ni kukagua yale waliyoahidi katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 kama yanatekelezwa.
Amesema hayo leo Jumatano Aprili 12, 2023 wakati kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mbozi na Kamati ya Usalama ya wilaya hiyo zilipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekekelezwa na Serikali katika wilaya hiyo.
Amesema kuwa kamati hiyo inatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuona utekelezaji wa ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza Serikali.
"Sasa hivi tunajiridhisha na kile tulichoahidi kuwa je kinafanywa na Serikali yetu ambayo tumeipa ridhaa ya kufanya hiyo kazi" amesema
Amewataka wananchi kuitunza miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali katika maeneo yao ili iwe na tija.
"Jukumu la kwanza la ulinzi wa miundombinu ni la mwananchi wa eneo husika, tulinde miundombinu yetu" amesisitiza.
Kamati hizo ambayo zimeanza ziara leo, zimetembeleza ujenzi wa barabara za Ilolo-Ndolezi, Hatelele-Iwezi na Isansa-Msanyila.
Pia kamati hizo zimetembelea na kukagua kituo cha Afya Ndolezi, mradi wa maji Mahenje na chanzo cha maji mto Isenga.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa