MBOZI. Wadau wa elimu Kata ya Idiwili wilayani Mbozi mkoani Songwe wamewekea mikakati mbalimbali itakayosaidia kuinua kiwango cha elimu katika kata hiyo.
Mikakati hiyo imefikia leo Jumamosi Februari 25, 2023 katika kikao cha wadau wa elimu katika kata hiyo.
Akitoa salamu kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo, afisa taaluma elimu msingi, Oswad Mwakabungila amesema kuwa mkurugenzi amemwagiza mambo manne.
Mwakabungila ametaja mambo hayo kuwa ni pamoja na utoaji wa chakula shuleni kuwa hilo sio ombi ni lazima.
"Kufuta KKK tatu, walimu wahakikikishe wanatokomesza uwepo wa wanafunzi ambao hawajui kusoma kuandika na kuhesabu na wahakikishe wanabandika ofisini ordha ya wanafunzi ambao hawajui kusoma orodha ofisini na chini ya majina yale iwepo mikakati ya kukablikiana na hiyo changamoto"amebainisha na kuongeza;
"Usimamizi wa pamoja miradi mbalimbali inayoletwa katika shule zetu maana bila kufanya hivyo ndio maana kunatokea kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hii kitu ambacho sio sawa"
Ofisa taaluma huyo ameongeza kuwa katika suala la taaluma Kata ya Idiwili haiko shwari hivyo wajitahidi ionekane wananapiga hatua.
"Mwaka huu matokeo hayatakuwa ya shule yatakuwa ya mwalimu binafsi kwahiyo ukifanya vibaya utawajibishwa wewe kama mwalimu" amesisitiza
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Christopher Ntandala amesema wapo tayari kupokea miradi itakayoletwa na serikali.
"Suala la chakula mimi pamoja na watendaji na wenyeviti wa vijiji nitahakikisha tunaongea na wananchi na baada ya wiki mbili tutatoa mrejesho" ameahidi diwani huyo.
Naye afisa elimu Kata ya Idiwili, Michael Nzunda amesema upendo na ushirikiano ndio vinainua elimu hivyo kuwataka kuwa na ushirikiano.
"Utoro wa walimu mahala pa kazi pia ni changamoto" ameeleza Nzunda
Ametoa wito kwa walimu kuwapa watoto mazoezi ya kutosha ili waweze kiluyakumbuka waliyofundishwa kupitia mazoezi hayo.
"Mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko tupige hatua tuweke mkazo katika hili, tumekubaliana kila mtihani tupige hatua na maelekezo yote tumeyapokea na tutayafanyia kazi na mrejesho tutawapatia" amesema
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa