• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

DKT MAHERA ATOA MAAGIZO WATUMISHI WA AFYA MKOA WA SONGWE

Kurushwa hewani: July 13th, 2023

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt Charles Mahera ametoa maagizo kwa watumishi wa afya katika Mkoa wa Songwe ambayo yatasaidia kutoa huduma bora kwa wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza na watumishi hao leo Alhamisi Julai 13, 2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt Mahera amesema kuwa lengo la Tamisemi ni kutoa huduma bora hivyo amewaagiza watumishi na viongozi katika sekta ya afya kuzingatia utawala bora.

“Sisi Tamisemi katika kitengo cha Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe tuna mpango mkakati kuanzia mwaka 2022/23 hadi 2025/26  wa kuchochea masuala ya utawala bora na ushirikishwaji wa jamii katika mfumo wa utawala. Ninyi kama viongozi mnatakiwa muwe na skills za leadership ndio maana tunatoa semina ili mtusaidie kutoa hizo huduma nzuri” amesema.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa jambo la pili ni kuhakikisha wananchi wengi wanapata huduma bora katika ngazi za chini katika maeneo yao.

“Tunataka watu wengi kwenye primary health ambazo ni zaidi ya Watanzania asilimia 80 hadi 90 ya Watanzania wanatibiwa. Ndio maana mnaona vituo na zahanati vimeshushwa huko chini na Serikali itaendelea kujenga na kuboresha vituo hivyo sasa tunawategemea ninyi zaidi” ameeleza

Amesema kuwa Serikali inapotimiza wajibu wake wa ujenzi wa vituo na kuboresha miundombinu inawategemea watumishi hao kusaidia kutoa huduma bora.

Jambo lingine ambalo Dk Mahere amewaagiza watumishi hao ni suala la mawasilano ambapo amewataka kutathimini namna wanavuyowasiliana na wagonywa au viongozi wanavyowasiliana na watumishi hao.

“Lakini tuna mifumo mingi ya Tehama tunataka itumike itusaidie kukusanya takwimu. Mhakikishe mnaweka kwenye mifumo takwimu sahihi na kwa wakati ili ziweze kuwasaidia kufanya mipangio vizuri” amesema

Amesema kuwa watumishi hao wanatakiwa kufanya tafiti mbalimbali huku viongozi wakitakiwa kusimamia vizuri watumishi wa kada hiyo ili kufikia matarajio ya viongozi wa kitaifa.

Aidha, Dk Mahera amesema kuwa Serikali inaendelea kutoa fedha katika sekta ya Afya ili kuweka mazingira bora ya kutoa huduma za kitabibu ambapo mkoa huo umepewa shilingi bilioni 5.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya katika halmashauri za mkoa wa Songwe.

“Msimamie vizuri fedha hizi zinazoletwa kwenu isiwe kama ni fursa ya kuweza kupiga. Masuala ya upigaji yamepitwa na wakati. Ukipiga utaumia. Mfanye matumizi mazuri ya dawa kwa sababu fedha nyingi zimeelekezwa huko kwa hiyo hakikisheni dawa zinawafikia walengwa” amesisitiza

Pia, Dk Mahera amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha masuala ya usafiri ambapo kila halmashauri itapewa magari matatu ikiwemo mawili ya kubebea wagonjwa.

“Tunaendelea kuboresha masuala ya usafiri ili watu wetu wale walioshindikana kutibiwa katika sehemu moja wapelekwe kwenye eneo jingine. Kuna magri 528 yanakuja, katika hayo ambulance zipo 316 hizi tutagawa katika kila halmashauri ambulance mbilimbili na hardtop mojamoja” amesema

Hata hivyo, Dk Mahera amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde kuwasimamisha kazi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi, Mganga Mfawidhi na Mfamasia ili kupisha uchunguzi wa mapungufu yaliyobainika katika hospitali hiyo.

“Watu watatu hao wasimamishwe, uchunguzi ufanyike ndani ya muda mfupi tupate taarifa. Tunaposema tunakusimamisha hatujasema tunakufukuza kazi, tunapomsimamisha isichukue muda mrefu. Ufanyike uchunguzi wa haraka ili mtu aweze kupata stahiki yake. Fanyeni uchunguzi wa haraka bila upendeleo” amesema.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo, Happiness Seneda amesema kuwa amepokea maelekeza hayo na kuahidi kuwa atakwenda kuyafanyia kazi na kuyasimamia.

“Tutakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika sekta hii. Watumishi nitawahamisha na nitawababilisha wa huku atakwenda huko lakini tutachunguza tukibaini umefanya ubadhirifu tutakufukuza kazi” ametahadharisha

Amesema kuwa watashirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha wanabaini wizi wa dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa