Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Kenani Kihongosi amewapongeza waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa kazi wanazoendelea kuzifanya katika Wilaya hiyo hasa ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mhe. Kenani ametoa pongezi alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt Francis Michael katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Oktoba 27,2023.
‘’Pamoja na majadiliano mtakayoyafanya kwa masilahi ya wananchi napenda kusisitiza mambo machache ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwani bila mapato nchi hawezi kupiga hatua na vilevile mapato yakusanywe kupitia mifumo ya Serikali kuhakikisha fedha zinafika sehemu husika’’ amesema
Ameongeza kuwa baadhi ya Halmashauri zimekuwa zikikusanya fedha mbichi, fedha za mikononi hali ambayo sio sahihi.
"Ili tuweze kupiga hatua vizuri ni lazima tubane matumizi na tukusanye mapato ya kutosha na dhamira njema itakuwa imetimia kwa watu waliotupa ridhaa ya kuongoza katika kata zetu, kwahiyo suala la mapato likawe ajenda ya kudumu na kama tunakusanya tutumie kwa uadilifu" amesisitiza
Jambo linguine alilosisitiza Mhe. Kihangosi ni usimamizi wa miradi ya maendeleo.
"Mheshimiwa Rais analeta fedha nyingi nyie wenyewe ni mashahidi katika miradi ya afya, elimu, maji, barabara umeme, sasa hapo kazi yetu ni kwenda kusimamia kuhakikisha thamani ya fedha inaendane na mradi;
Msikubali kupokea miradi iliyochini ya kiwango kwa maana mainjinia wetu wawe wanafika saiti kusimamia miradi, tumeajiriwa tunalipwa mishahara kwaajili ya umma kwahiyo kila mmoja akatimize wajibu wake".
"Tusimamie suala la usafi wa mazingira, utupaji taka ovyo, uchomaji misitu, ufyekaji misitu bila utaratibu bila kufanya hivi tutajikuta tunaingia kwenye ukame, magonjwa ya mlipuko"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa