• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

DC Mbozi aomba ushirikiano, amshukuru Rais Samia

Kurushwa hewani: January 30th, 2023

Mbozi. Siku sita baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya nchini, mkuu mpya wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Esther Mahawe amewaomba ushirikiano watumishi wa halmashauri hiyo huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi nyingine ya kuendelea kuongoza katika Wilaya ya Mbozi.


DC Esther ni miongoni mwa wakuu wa wilaya waliohamishwa katika mabadiliko ya wakuu wa wilaya yaliyofanya na Rais Samia Januari 25 mwaka huu akihamishwa kutoka wilaya ya Kigoma na kupelekwa Wilaya ya Mbozi.


Katika mabadiliko hayo, Rais Samia aliteua wakuu wa wilaya wapya 37, kuhamisha wakuu wa wilaya 48 huku wengine 55 wakiendelea kuongoza katika wilaya zao.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 30, 2023 wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa mkuu wilaya hiyo, Cosmas Nshenye, mkuu huyo wa wilaya mpya amesema "Namshukuru mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kunipa kipande kingine cha kuendelea kuongoza katika Wilaya ya Mbozi"


"Nawashukuru wote kwa kunikaribisha nimetokea eneo ambalo ni mpakani kama huku tu, mimi ni kiongozi sio mtawala naomba ushirikiano wenu ilituweze kulijenga taifa letu kwa pamoja,


Kwa kifupi mimi ni DC wa kwenda field kwenda kuangalia nini kinafanyika na kisikiliza kero za wananchi nikikiwa field hukohuko" amesema mkuu huyo wa wilaya.


Amesema kuwa katika  kutekeleza miradi ya serikali hatakuwa na mzaha.


"Katika kutekeleza miradi serikali sitakuwa na mzaha ikitekelezwa kwa kusuasua, naomba mnielewe kama mimi ni mtu ninayezingatia viwango" ameweka wazi DC huyo mpya wa Wilaya ya Mbozi ambaye amehamishwa kutoka Wilaya ya Kigoma.


 Nshenye awataka Mbozi kuendelea kuhubiri upendo


Katika makabidhiano hayo, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Cosmas Nshenye amewataka watumishi na wananchi wa halmashauri hiyo kuendelea kudumisha upendo na mahusiano mazuri.


Nshenye amesema kuwa ameacha kiporo cha kuwakutanisha watu wa imani tofauti katika sala ya pamoja ili waweze kuwa na upendo.


"Nimeondoka nimeiacha kiporo kuwakutanisha watu waimani tofauti kukutana katika sala ya pamoja hata mara moja kwa mwezi ili watu waweze kuwa na upendo ili kama suluhu ya baadhi ya matatizo" amesema Nshenya


Nshenye amewashukuru viongozi wa kimila na viongozi wa dini kwa kufanya nao kazi kwa ukaribu pamoja na viongozi wa siasa na taasisi za

Serikali.


Pia, amewaomba watumishi kuwa na maandalizi ya kustaafu akiwataka kuwa na mahusiano mazuri na wanajamii.


"Ukiwa na mahusiano mazuri nawatu huko mtaani pindi ukiwa kazini ukirudi huko hautapata shida hivyo bila kujali una umri gani ujiandae kustaafu" amedokeza


"Ombi langu muendelee kuhubiri upendo, masuala ya ukatili hayatakuwepo,


Naaga leo Mbozi sio kwamba naondoka moja kwa moja nitarudi kuwasalimia" ameahidi Nshenye.


DAS ataja watakayokumbuka kwa Nshenye


Akizungumzia namna watakavyo mkumbuka aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi (DAS), Tusubilege Benjamini amesema kuwa Nshenye alikuwa kama mzazi anayewaelekeza watoto wake.


"Alikuwa kama baba maana mimi na mkurugenzi alikua anaongea na sisi kama watoto wake,


Amesema kuwa Nshenye aliweza kutatua migogoro mingi ambayo ilikuwa imedumu kwa miaka mingi.


"Alikua anatatua migogoro ambayo imeshindikana miaka mingi katika wilaya ya mbozi tutamkumbuka kwa hilo,


Aliinua vipato vya kinamama kwa kuhamasisha kuwaunga mkono wakinamama wanaozalisha batiki katika vikundi batiki zao kutumika katika sherehe mbalimbali kama vile Mwenge wa Uhuru" amesema katibu tawala huyo wa wilaya na kuongeza;


"Idara ya maendeleo ya jamii waendelee kuwaunga mkono wakinamama katika vikundi vyao"


Tutakukumbuka sana kwa busara na hekima zako katika kufanya maamuzi mbalimbali, kuishi vizuri na watumishi pamoja na wanajamii kwatika wilaya yetu umekuwa mfano mzuri wa kuigwa" ameeleza DAS  huyo.


 Atatua mgogoro uliodumu miaka 25

*


Akizungumza kwa niaba ya kamati ya amani ya wilaya hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya amani, mzee Salehe  Simba amesema kuwa Nshenye ni DC wa kipekee aliyewahi kutatua mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka 25 ambapo wenzake hawakuweza.


"Nshenye ni DC wa kipekee aliyewahi kutatua mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka 25 ambapo wenzake hawakuweza" amesema mzee Simba  kwa niaba ya kamati ya amani ya wilaya.


"Tutamkumbuka kwa busara nyingi sana alizojaliwa na kwakwe kulikuwa hakuna kitu kilichoshindikana hata kama kwako unaliona nitatizo kubwa lakini likifika kwake utaliona dogo sana" ameeleza

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa