Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Hamadi Mbega amewataka Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha mafunzo waliyoyapata katika ziara ya kujifunza katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro yanaleta tija kwa wananchi wa Mbozi.
Mhe. Mbega ametoa rai hiyo leo Jumanne Februari 25, 2025 wakati alipoongoza Kamati hiyo katika ziara ya kujifunza ambapo wametembelea miradi ya kimkakati katika Manispaa ya Morogoro, lengo likiwa ni kujifunza uendeshaji wa miradi hiyo ili kuongeza mapato.
Katika ziara hiyo, Kamati ilipata fursa ya kujifunza kuhusu mbinu zilizotumika katika miradi ya kimkakati kwa mafanikio, ikiwa ni pamoja na ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).
Mhe. Mbega amepongeza jitihada za Manispaa ya Morogoro kwa kuweza kuibua na kusimamia miradi ya kimkakati ikiwemo Jengo la Kitega Uchumi la Manispaa, Soko Kuu la Chifu Kingalu lililojengwa kwaajili ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa pamoja na Stendi Kuu ya Mabasi Msamvu.
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema kuwa anaamini mafunzo hayo yataleta tija kwa Kamati ya Fedha na Uongozi pamoja na Wataalamu walioshiriki katika mafunzo hayo.
Kamati hiyo ya Fedha ilianza ziara ya kujifunza jana Jumatatu Februari 24, 2025 katika Manispaa ya Temeke kisha leo katika Manispaa ya Morogoro.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa