Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega amewaagiza watendaji kata, watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji kuhakikisha vitendo vya uharibifu wa mazingira vikiwemo ukataji miti na uchomaji mkaa vinatokomezwa katika maeneo yao huku akitoa wiki moja kwa watendaji wa kata ambazo uharibufu wa mazingira umekidhiri kufanya mabadiliko ya kudhibiti uharibifu huo.
Amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo utakuwa kipimo kwao kama wanatosha kwenye nafasia zao na kama hawatabadilika ataagiza wachukuliwe hatua za kinidhamu.
Mhe. Mbega ametoa maagizo hayo leo Jumatatu Machi 10, 2025 wakati wa kikao maalumu cha kupanga mikakati ya namna ya kudhibiti ukataji miti, uharibifu wa misitu na uchomaji mkaa katika Wilaya hiyo kilichowahusisha Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalamu kutoka Idara ya Maliasili na Mazingira, TFS, Watendaji wa Kata 12, watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji vya kata 12 ambazo uharibifu wa mazingira umekidhiri.
Amesema kuwa kikao hicho kimekuja baada ya ziara iliyofanywa na Kamati ya Usalama ya Wilaya kuona na kufanya tathimini ya hali ya uharibifu wa mazingira, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo wakati akimwapisha Mkuu wa Wilaya huyo.
DC Mbega amesema kuwa baada ya kufanya ziara Kamati ya Usalama ilibaini kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kata nne unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya uchomaji mkaa pamoja na shughuli za kilimo.
“Ukataji wa miti ni jambo ambalo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan analikemea lakini pia Mkuu wetu wa Mkoa (Mhe. Daniel Chongolo) wakati ananiapisha aliniambia jukumu la kwanza changamoto iliyo katika Wilaya yetu ya Mbozi ni ukataji wa miti na uuzaji wa mkaa ni jambo ambalo unapaswa kulishughulikia na maelekezo yale alinipa mimi lakini yanatakiwa yashuke mpaka huku chini kwenu (watendaji wa kata). Kwa hiyo watendaji kata na vijiji mnajukumu la kuhakikisha uharibifu wa mazingira haupo” amesema
Amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeanzisha mpango maalumu wa ugawaji wa mitungi ya gesi bei nafuu
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa