Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega amefanya ziara maalumu katika eneo la kihistoria la Kimondo lililopo wilayani humo ikiwa ni mwendelezo wa ziara wa kutembelea taasisi za umma
zilizopo wilayani humo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mbega amebainisha kuwa eneo la Kimondo ni urithi wa thamani kwa taifa na lina nafasi kubwa katika kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi.
Amesisitiza kwamba juhudi za pamoja zinahitajika ili kuhakikisha eneo hilo linaendelea kuhifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Mhe. Mbega ametoa wito kwa jamii inayozunguka eneo hilo kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi katika kulinda na kutunza kivutio hicho.
Kimondo cha Mbozi ni moja ya kimondo kikubwa duniani na kufanya kuwa kivutio cha kipekee kwa wanasayansi, wanahistoria, na watalii Mamlaka ya Ngorongoro, inayosimamia eneo hilo, imeweka juhudi kubwa kuhakikisha urithi huu unaendelea kuwa kivutio cha kimataifa.
Mhe. Mbega amesisitiza kuendelea kuhifadhi mazingira, na uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda urithi wa taifa.
Ameahidi kushirikiana na mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza ili kuboresha uzoefu wa watalii na kuongeza mapato ya wilaya na Taifa kwa kwa ujumla
Aidha, ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Ngorongoro kwa kazi nzuri ya kusimamia eneo hilo na kuhakikisha linaendelea kuwa salama.
Wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya alikutana watumishi wa eneo hilo na baadhi ya viongozi wa kata ya Mlangali na kuzungumza nao mazungumzo yao yalilenga kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha eneo hilo na kuongeza idadi ya watalii.
Pia, aliwahimiza wananchi kuona umuhimu wa utalii kama moja ya njia za kuimarisha maisha yao kupitia fursa za ajira na biashara.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa