Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamadi Mbega amwemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.
Hafla hiyo imefanyika Ijumaa Januari 31, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe iliyopo Mji wa Vwawa, Wilayani Mbozi.
Katika hafla hiyo, Mhe. Mbega amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuboresha miundombinu hasa katika sekta ya afya.
Mkuu wa Wilaya huyo ameeleza kuwa lengo la kuzindua Bodi hiyo ni kuboresha utoaji wa huduma bora na utawala bora katika hospitali pamoja na kusimamia rasilimali zilizopo.
"Bodi itashughulikia matumizi sahihi ya fedha kwa kuzingatia vipaumbele katika utoaji wa huduma kwa wananchi, itapokea na kujadili taarifa za fedha pamoja na taarifa za utoaji wa huduma za afya ili kuweka taasisi katika hali salama" ameeleza
Amesisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu, ikiwemo huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.
Kwa kipindi cha miaka 2019 hadi 2024, jumla ya Shilingi bilioni 16 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya hospitali hiyo.
Miundombinu hiyo inajumuisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la huduma za maabara, jengo la mama na mtoto, jengo la wagonjwa mahututi (ICU), jengo la wagonjwa wa dharura, nyumba ya mtumishi, na mradi wa DST ambapo majengo yote hayo yamekamilika na yanatoa huduma.
Aidha, Kwa mwaka wa Fedha 2023/24, hospitali imetumia zaidi ya Shilingi milioni 171 katika ujenzi wa jengo la ndugu kusubiri, kichomea taka, na ujenzi wa njia za watembea kwa miguu.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa