Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega amefanya ziara maalumu ya kuwatembelea viongozi wa dini katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za kidini.
Mhe. Mbega amefanya ziara hiyo leo Jumanne Februari 4, 2025 ikiwa na lengo la kuimarisha mshikamano wa kijamii, kudumisha amani, na kushirikiana katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, DC Mbega amewaeleza viongozi wa dini kuwa ushirikiano baina yao na Serikali ni muhimu kwa ustawi wa jamii.
"Viongozi wa dini mna nafasi kubwa katika malezi ya maadili, kuhamasisha maendeleo, na kuimarisha amani katika jamii" amesema
Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza umuhimu wa viongozi wa dini kuwa sehemu ya juhudi za kupambana na changamoto kama vile umaskini, ukosefu wa elimu, na mmomonyoko wa maadili.
Ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa taasisi za kidini katika utoaji wa huduma muhimu kama elimu, afya, na misaada ya kijamii.
Kwa upande wa viongozi wa dini wampongeza Mkuu wa Wilaya kwa juhudi zake za kushirikiana na jamii ya kidini.
Wamesema kuwa wako tayari kuunga mkono mipango ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi wa Mbozi.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa