Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Esther Mahawe amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kupanda miti katika kaya zao ili kuepuka athari za kimazingira zinazoweza kujitokeza kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira iliopo hivi sasa
Rai hiyo ameitoa leo ijumaa Disemba 8, 2023 wakati wa maadhimisho wa Siku ya Maadili Duniani ambayo huaadhimishwa kitaifa kila tarehe 10 Disemba.
Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa Serikali imeelekeza kupanda miti mitano kwa kaya za mjini na miti 10 kwa kaya za vijijini.
"Napenda nitumie fursa hii ya maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kuwashawishi tuendelee kupanda miti. Lakini twendeni pia katika kaya zetu tukapande miti ni kwa faida yenu ndugu zangu mazingira hayachezewi yakikasirika tutajutia" amesema na kuongeza;
"Viongozi wa vijijini nitoe rai kupitia maadhimisho haya wapate taarifa hii nimeambiwa kuna baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wao ni vinara wakuuza maeneo ya milimani na maeneo ya misitu"
"Ninayo majina yao na wiki ijao naanza kufuatilia kijiji kwa kijiji wanauza ardhi ovyo, wanaruhusu watu kulima katika milima;
Naomba watu wa misitu nendeni kawekeni makatazo ya mabango katika maeneo hayo ila mazingira yasizidi kuharibiwa" amesema
Mhe. Mahawe amewapongeza viongozi ambao ni waadilifu ambao wanasimamia vizuri mazingira wakishirikiana na wananchi wao.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa