Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Esther Mahawe amewataka watumish i wa afya katika Hospitali ya Wilaya hiyo Vwawa kufanya kazi kwa weledi ili kuokoa maisha ya watu huku akisema wahudumu hao ni mashujaa.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa rai hiyo leo Jumanne Julai 25, 2023 baada ya kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi-Vwawa ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashuja.
DC Mahawe ambaye ameongoza watumishi mbalimbali wa wilaya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika zoezi hilo amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi kutokana na mkoa huo kutokuwa na mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Amesema kuwa watumishi wa afya hasa matabibu wanapokea watu wengi wakiwemo wagonjwa hivyo amewaasa kufanya kazi kwa weledi ili kuokoa maisha yao.
“Mimi niwapongeze na kuwashukuru. Tuendelee kutekeleza majukumu yetu hasa ninyi matabibu muendelee kufanya kazi zenu kwa weledi ili kuokoa maisha ya watu wengi wanaoletwa mikononi mwenu. Mungu awabariki sana” amesema DC Mahawe na kuongeza;
“Tunajua mpango wa kufa ni wa Mungu lakini ninyi mnaweza kuokoa maisha ya mtu ili asife kizembe kwa sababu ninyi ni matabibu wa duniani hivyo ninyi ni mashujaa na tunatambua jitihada zenu” amesema
Pia, Mkuu huyo wa Wilaya amewashukuru watumishi wote waliojitokeza kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Awali akizungumza baada ya zoezi hilo la usafi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbozi Majaliwa Mlawizi amesema kuwa watumishi wa afya ni mashujaa ambao wanaokoa maisha ya watu hivyo kada hiyo ni muhimu sana.
“Tumaeamua kuja kufanya usafi katika eneo la hospitali. Hapa napo kuna mashujaaa. Mashujaa hawa wanapambana katika kuokoa maisha ya wananchi.
“Mimi nitoe rai kwa wahudumu maisha yetu tunapokuwa tunafika hapa yako mikononi mwenu. Fanyeni kazi kwa weledi” amesema
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa