MBOZI. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wake wa miradi ya maji ambayo inasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa maji na kumtua mama ndoo kichwani.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa shukrani hizo mbele ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Nselewa-Mlowo inayofanyika katika uwanja wa Karasha kata ya Mlowo Wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Akizungumza katika hafla hiyo, DC Mahawe amesema Rais Samia amezidi kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inawatatulia changamoto wananchi.
"Tunamshukuru sana mama Samia kwa kuendelea na kazi kubwa ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kutekeleza miradi ya Maji, tunaomba ufikishe shukrani hizi kwa Rais Samia" amesema DC Mahawe mbele ya Waziri Aweso.
Waziri Aweso yuko kwenye ziara ya siku moja mkoani Songwe ambapo amezindua mradi wa maji ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Waziri Aweso amezindua mradi huo utakaohudumia zaidi ya wananchi 15,504 wa kata ya Vwawa na Mlowo wilayani Mbozi mkoa wa Songwe
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa