Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Mh Esther Mahawe amesema kuwa Mwenge wa Uhuru 2023 utakimbizwa kilomita 154 huku ukipitia miradi nane yenye thamani ya Sh8.2 bilioni katika Wilaya hiyo.
DC Mahawe amesema hayo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 baada ya kupokea Mwenge huo katika Kijiji cha Nanyala kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mh Solomon Itunda.
Wilaya ya Mbozi inakuwa ya tatu kupokea Mwenge huo leo ambapo utakimbizwa na kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo kabla ya kukabidhiwa Halmashauri ya Mji Tunduma kesho.
Akizungumza katika mapokezi hayo kiwilaya, Mkuu huyo wa Wilaya amesema "Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Mbozi utakimbizwa Kilometa 154 na utapita katika miradi nane yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8.2 " amesema Mh Mahawe
"Ninaahidi kwa kipindi chote Mwenge wa Uhuru utakapokuwa hapa Songwe tutaulinda, tutautunza pamoja na wakimbiza Mwenge wote. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie"
Mwenge wa Uhuru ulipokewa kimkoa Jumamosi Septemba 2 mwaka huu katika kijiji cha Kamsamba Wilayani Momba na unatarajiwa kukabidhiwa Mkoa wa Mbeya Septemba 7 mwaka huu.
Akizungumza katika mapokezi ya Mwenge huo kimkoa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh Dk Francis Michael alieleza kuwa Mwenge huo utakimbizwa Kilometa 722 na kupotia miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 15.5
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa